Kulingana na vyombo vya habari nchini Kenya naibu kiongozi wa chama cha Orange Democratic Party (ODM) Wycliffe Oparanya na kiongozi wa Chama cha Roots George Wajackoyah walilazimika kukimbia kutafuta usalama huku polisi huko Bumala, kaunti ya Busia wakiwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali.
Wawili hao walikuwa wakiongoza maandamano hayo Jumatano, Julai,12 katika mji wa Busia.
Oparanya na Wajackoya walikuwa wakikusanya watu kukusanya saini za mpango wa ‘Tumechoka’ ambao ulizinduliwa na kiongozi wa chama cha Azimio, Raila Odinga ikiwa ni hatua ya kumtimua Rais William Ruto afisini.
“Tutaandamana hadi gharama ya juu ya maisha nchini Kenya ishughulikiwe,” Oparanya alisema wakati wa maandamano hayo.