Ni Julai 12, 2023, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ambae amekutana na Vyombo vya Habari kuhusu suala la Uwekezaji wa Bandari.
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati za Kudumu ya Bunge, hata huko baadae mtaambiwa Bandari mwaka huu imeendelea kuvunja rekodi ya makusanyo, lakini bado haitoshi. Mnaopita bararabani kule Barack Obama, mnaona meli zimepaki zinataka kushusha mzigo’- Jerry Silaa Mbunge Ukonga.
‘Msidhani kusimama zinapenda, zinasubiri zamu ya kuingia nangani kushusha mzigo. Leo mfanyabiashara yoyote tunayemuhudumia akiulizwa, anajibu anaweza kujua jinsi ya kufika bandarini, lakini hawezi kusema lini atashusha mzigo kwa sababu ya ucheleweshaji na wao kujikuta wakilipa Milioni 60 hadi 90 ya ucheleweshaji huo na kuongeza gharama kubwa kwa walaji,” Jerry Silaa Mbunge Ukonga.