ulingana na chanzo cha habari cha nchini Kenya kimesema idadi ya waliofariki katika mauaji ya ibada ya Shakahola imeongezeka hadi 372 baada ya miili 12 zaidi kufukuliwa Jumatano, Julai,12, siku ya tatu ya awamu ya nne ya operesheni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha alisema jumla ya waliookolewa wamesalia 95 tangu operesheni hiyo ilipoanza Aprili.
Onyancha pia alisema kuwa hakuna watu wapya waliokamatwa, na hivyo kubakiza idadi ya waliokamatwa wakiwa 37.
Haya yanajiri siku moja baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kufika mbele ya kamati ya seneti inayohusika na kesi ya mauaji ya Shakola.
Waziri wa Mambo ya Ndani alisema kuwa serikali itashinikiza mageuzi ya kisheria ili kuwadhibiti wahubiri wahuni nchini.
TAZAMA PIA;