Jordan Henderson amekubali pendekezo la Al Ettifaq inasemekana kuna makubaliano ya maneno kwa kanuni na mkataba ulikubaliwa.
Hayo ni kwa mujibu wa Fabrizio Romano, ambaye ameripoti ‘makubaliano ya mdomo’ yapo kati ya klabu hiyo ya Saudi Arabia na nahodha huyo wa Liverpool.
Jurgen Klopp anadaiwa kumpa Henderson ‘taa ya kijani’ kuondoka.
Dili sasa inategemea Liverpool na Al Ettifaq kujadili juu ya ada, hakuna nafasi ya kumwacha aondoke bure.
Iwapo Jordan Henderson ataenda Saudia kwa inasemekana gharama yake ni £700,000 kwa wiki kiungo huku klabu ya Saudi Pro League, Al-Ettifaq ikitaja kuwa tayari kuongeza mshahara wake karibu mara nne
Jordan Henderson bado ni mchezaji muhimu wa Liverpool na England.