Ulimwengu umeungana kuchangia dhamira ya kukomesha janga la UKIMWI kama tishio kwa afya ya umma ifikapo 2030 na imekubali maono ya UNAIDS ya [zero HIV] na kukomesha vifo vinavyohusiana na UKIMWI na kukomesha ubaguzi.
Ugonjwa huo hatari ulioua watu milioni 40.4 tangu kuanza kwa janga hilo mwaka 1981.
“Takwimu katika ripoti hii zinaonyesha kuwa njia inayomaliza Ukimwi sio siri, lakini ni chaguo. Ni chaguo la kisiasa na kifedha,” alisema Winnie Byanyima, mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS
Virusi vya HIV na Ukimwi vinaweza kumalizika kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 kama mataifa yanaweza kuwa na utashi wa kisiasa na msaada muhimu wa kifedha ili kuushinda kabisa, ripoti mpya iliyochapishwa Alhamisi inasema.
Ugonjwa huo hatari umeua watu milioni 40.4 tangu kuanza kwa janga hilo mwaka 1981. “Takwimu katika ripoti hii zinaonyesha kuwa njia inayomaliza Ukimwi sio siri, lakini ni chaguo. Ni chaguo la kisiasa na kifedha,” alisema Winnie Byanyima, mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS.
“Ripoti hiyo inaonyesha kuwa majibu ya HIV yanaweza kufanikiwa wakati yanatia nanga katika uongozi imara wa kisiasa,” alisema.