Bodi ya kitaifa ya Chama cha Waigizaji wa Marekani ,Shirikisho la Wasanii wa Televisheni na Redio (SAG-AFTRA) lilipiga kura Alhamisi kugoma, na kuwaita wanachama wake 160,000 kuandamana , maafisa wa chama walisema.
Bodi ya kitaifa ilipiga kura kwa kauli moja kuendelea na mgomo, alisema Duncan Crabtree-Ireland, mkurugenzi mtendaji wa kitaifa wa muungano na mpatanishi mkuu na alisema wanachama wa chama hicho wataanza kugoma usiku wa manane Alhamisi na kutoa wito kwa wanachama kujiunga na maandamano hayo Ijumaa asubuhi.
Chama cha Waigizaji (SAG) kinawataka wasanii wakubwa wa kanda za moja kwa moja kukubali mgao mzuri wa faida na mazingira bora ya kufanya kazi.
Kusimama kwao kufanya kazi kunamaanisha kuwa idadi kubwa ya filamu na utayarishaji wa TV za Marekani utasimama.
Nyota Cillian Murphy, Matt Damon na Emily Blunt waliondoka kwenye onyesho la kwanza la Oppenheimer ya Christopher Nolan mjini London Alhamisi usiku wakati mgomo huo ulipotangazwa.
Mgomo huo wa SAG unaanza saa sita usiku saa za Los Angeles (08:00 BST). Maandamano yataanza Ijumaa alfajiri nje ya makao makuu ya California ya Netflix, kabla ya kuelekea Paramount, Warner Bros na Disney.
Muungano huo – unaojulikana rasmi kama Chama cha Waigizaji -Shirikisho la Wasanii wa Televisheni na Redio Marekani, au SAG-AFTRA – pia unataka uhakikisho kwamba akili bandia (AI) na nyuso na sauti zinazozalishwa na kompyuta hazitatumika kuchukua nafasi za waigizaji.