Licha ya kuwepo kwa Changamoto mbalimbali katika Jimbo la Busanda Halmashauri ya wilaya ya Geita Baadhi ya wananchi katika kata ya Nyamalimbe kijiji cha Lwamawazo wameulalamikia Uongozi wa Kata hiyo kushindwa kuweka wazi Fidia ambazo zimekuwa zikitozwa kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakikiuka Maadili.
Hayo yameelezwa na Wananchi wa kata hiyo katika Mkutano ambao uliandaliwa na Mh.Mbunge wa Jimbo hilo Mhandisi Tumain Magesa katika kujibu kero na kutatua, sambamba na kutembelea Miradi ambayo imekuwa ikitekelezwa katika Jimbo lake la Busanda huku wakimtaka Mhandisi Magesa kufanya uchunguzi wa kina .
Mhandisi Tumain Magesa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi, Tumain Magesa amesema ataviomba vyombo pamoja na Mamlaka kwa ajili ya kuja kuchunguza tuhuma hizo ambazo zimekuwa zikiwakabili Uongozi wa kata hiyo.