Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amesema mchakato wa kuipata Kampuni ya DP World ulifanyika baada ya kuzichuja kampuni saba kutoka Nchi mbalimbali duniani na kwamba Serikali ilianza majadiliano na DP World kutokana na kuwa na vigezo zaidi ya kampuni nyingine zilizotuma maombi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es salaam.
“DP World ina uwezo mkubwa wa kuendesha Bandari Afrika, Asia, Ulaya na America , DP World inamiliki zaidi ya Meli 400 za mizigo hii inaongeza ufanisi mkubwa katika usafirishaji wa mizigo, Wawekezaji wengine kutoka Singapore, Denmark, Ufaransa, Hongkok n.k hawakukidhi sifa za Mwekezaji mahiri ambaye anahitajika kwa Bandari ya Dar es salaam kwasababu hawakuwa na uwezo wa uchagizaji wa mnyororo mzima wa usafirishaji wa mizigo”
“Makubaliano haya Tanzania na Dubai hayana masharti yanayoifunga Serikali kuhusu maeneo ya ushirikiano yaliyoanishwa pasipokuwepo na mikataba mahsusi ya utekelezaji wa miradi itakayojadiliwa na kukubaliwa na pande zote mbili” ——— Profesa Mbarawa akiwa Dar es salaam leo.