Mahakama ya Kikatiba ya Afrika Kusini imeamua kuachiliwa mapema kwa Rais wa zamani Jacob Zuma kutoka gerezani kwa madai ya hali ya kiafya ilikuwa kinyume cha sheria.
Mnamo 2021, Zuma aliachiliwa kutoka gerezani chini ya wiki nane baada ya kuanza kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama na hayo yalijiri baada ya kukataa kutoa ushahidi wake katika uchunguzi dhidi ya ufisadi uliofanyika alipokuwa afisini.
Parole ya matibabu ya Zuma ilitolewa na huduma ya magereza, ikiongozwa na Arthur Fraser, mshirika wa rais wa zamani.
Haijabainika mara moja baada ya uamuzi huo wa Alhamisi ikiwa kurejea kwa rais huyo wa zamani kulikuwa kumekaribia.
Zaidi ya watu 300 walikufa katika ghasia zilizosababishwa na kukamatwa kwa Zuma.
Kwa mujibu wa Wakfu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini,Zuma atarejea nchini mwake wakati ambapo madaktari wake watakuwa wamemaliza kumhudumia.
Rais huyo wa zamani alisafiri kwenda Urusi kwa kutumia ndege ya umma wiki iliyopita kwa mujibu wa msemaji wa wakfu huo Mzwanele Manyi.