Usiku wa Julai 14, 2023 ambapo Ni Dj kutokea Afrika Kusini, Tyler ICU alitoa burudani ya nyimbo zao zinazotambulika kwa jina la Amapiano.
Mkali huyo alitumia zaidi ya masaa mawili kuwaburudisha mashabiki na wapenzi wa nyimbo hizo katika chimbo liitwalo Elements BAR masaki Dar es Salaam.
Millardayo.com & Ayo TV ilimpata Meneja wa Elements Bar, Makenzi aliyazungumza haya…’Kiukweli tunawashukuru wote waliofika kwani hii ni kubwa sana pia tunamshukuru Amour kwani ndio waandaji wa hii Event rekodi imeandikwa Dj amezicheza nyimbo, watu wamefurahi haijawahi kutokea kwa umati uliofika ni mkubwa sana watu wameitikia na milango iko wazi karibuni tuwahudumie kuanzia Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi’
Mbali na Meneja wa Elements lakini pia tulimpata Amour Shamtee ambae ndio alihusika kuandaa ama kumleta Tyler ICU lengo burudani hiyo iambatane na utambulisho wa kinywaji chake kipya kiitwacho Johari Gin.
‘Lengo langu ni Utambulisho wa Johari Gin uwafikia watu wote hivyo utambulisho utakuwa unaambatana na Dj’s ama Msanii na hapa ndio tumeanza hii ni kama trailer tu na hapa Elements watu wameitikia kwelikweli kwahiyo ni kubwa sana hii nimekuwa surprised kwa vibe la watu nimeamini Amapiano inapendwa na siku zijazo tutawajuza mashabiki nani anafuata kwani huu ni mwendelezo wa utambulisho wa Johari Gin ukiambatanishwa na burudani’- Mkurugenzi wa Johari Gin, Amour Shamtee
Hapa unaweza ukatazama baadhi ya picha ushuhudie kile kilichojiri Usiku wa Tyler ICU Elements Masaki Jijini Dar es Salaam.