Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndugu MOHAMMED ALI KAWAIDA (MCC) akizungumza na waandishi wa habari kuonesha msimamo wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM yakuwa unaunga mkono hoja ya Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Mkutano huo umefanyika kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Upanga Jijini Dar es Salaam 15 Julai, 2023.
Aidha Ndg, Kawaida, amesisitiza kuwepo kwa Maandamano ya Amani ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya Bandari nchini. Maandamano hayo yatafanyika nchi nzima ambapo yatazinduliwa rasmi Mkoani Dar es Salaam siku ya tarehe 18 Julai, 2023.