Baada ya mchezaji Clatous Chama kugoma kusafiri kuelekea Uturuki katika kambi ya Simba SC ya maandalizi ya msimu mpya 2023/24 alitarajia asafari ya Kundi la pili la Wachezaji.
Chama alitarajiwa aondoke leo alfajiri pamoja na Che Malone, Onana na Baleke lakini aligoma na hakuondoka na wenzake kwa kile kinachodaiwa ni kushinikiza kuboreshwa maslahi zaidi katika mkataba wake.
Baada ya kugoma huko kwa mara ya pili Muwekezaji wa Simba SC MO Dewji ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe ambao unaashiria kumlenga Chama.
Hata hivyo dakika chache baada ya ujumbe huo wa MO Dewji taarifa za chini ya kapeti zikadai Viongozi wa Simba na Chama wameafikiana na Chama sasa ataondoka na Mchezaji mpya wa Simba Fabrice Ngoma aliyesalia kushughulikia masuala ya visa.
Kwa habari kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi