Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Geita limesema limebaini uwepo wa Watu wanaoiba nyaya za transfoma na kuisababisha TANESCO hasara na baadhi ya Watu kukosa umeme huku wakiwataka wanaofanya hivyo waache tabia hiyo.
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Geita Mhandisi Michael Mbwana amesema kuna wimbi kubwa la wizi wa nyaya ambazo jukumu lake ni kulinda transfoma.
Mhandisi Mbwana amesema endapo tatizo la wizi wa nyaya hizo litakuwa endelevu ikitokea hitilafu itasababisha kuungua kwa transfoma sambamba na Wananchi kukosa umeme huku akiwataka Wananchi kulinda miundombinu hiyo.