Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, amefariki Dunia katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es salaam, ambako alikuwa akipatiwa matibabu na maziko yake yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni Zanzibar.
Mkurugenzi wa sasa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit Idarous Faina amethibitisha kifo cha Jecha na kusema “”Ni kweli Jecha amefariki na tunasubiri mwili wa marehemu kutoka Dar es salaam na kuwasilishwa hapa Unguja kwa ajili ya mazishi leo saa 10 jioni”
“Sisi kama ZEC tutamkumbuka juu ya ushirikiano wake na kutujenga kama Wafanyakazi kuwa kitu kimoja na kuwa na Falsafa yake kwamba Mkubwa yoyote ili athaminiwe aanze kumuheshimu Mdogo, hakuwa Mkali kwasababu ni Kiongozi alikuwa sana ni Mtu wa kuelekeza likitokea tatizo huelekeza na hatua za mwisho sana ndio utamkuta katika hali ya kukasirika lakini ni Mtu alikuwa so charming Mungu amlaze mahali pema InshaAllah”
Akiwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha atakumbukwa kwa maamuzi ya kufuta Matokeo ya Uchaguzi Zanzibae mwaka 2015 akidai Uchaguzi huo haukuwa huru na gaki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa Sheria za Uchaguzi.