Ni muda mwingine tena wa Rapper Young Dee ( @youngdaresalama ) kupita na maokoto yake baada ya ukimya wa zaidi ya mwaka mmoja bila kuachia goma lolote lakini sasa amewa-bless Raia na kitu kipya kinaitwa ‘basupa’ ft. @djallybi kinachopatikana kwa audio kwenye platform mbalimbali.
Flow zake, uandishi wake na level yake ya kupita juu ya mdundo wowote ndio vimemfanya kuendelea kuishi kwenye playlist zetu hata kama hana goma jipya na sasa leo ni siku rasmi ya kuanza kutetema na hili dude lake jipya la ‘basupa’ ambalo video yake inatoka wiki ijayo.
Jina lake lilianza kuhesabiwa kwenye Top 10 za fleva za Bongo na kuanza ku-shine toka mwaka 2009 alipomaliza kidato cha nne na kuachia ngoma yake ya ‘Teacher’ japo ngoma yake ya kwanza kuitoa ilikua ‘tafsiri’ ambayo aliiachia mwaka 2007 akiwa bado Mwanafunzi.
Kuanzia sasa na kuendelea nitakua nakuwekea ngoma mpya za Wakali wa Bongo mida ya asubuhi ili uishibishe playlist yako na pini mpya.……. kama kwa kipisi hiki tu umekubali jinsi Young D alivyopita na huo mdundo dondosha emoji yoyote nzito iliyokaribu nawe