Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue afunguka kuhusu uwepo wa utiri wa majeshi. Amesema hayo leo tarehe 20 julai 2023, wakati akizungumza na Wahariri Ikulu Jijini Dar-es Salaam.
“Kimsingi Jeshi kwenye nchi linakuwa ni Jeshi moja lakini sisi tuna majeshi mengi na inawachanganya Wananchi, inaongeza gharama kwa Serikali, silaha zinakuwa mikono mwa watu wengi na vitu vya namna hiyo”
“Lakini tutowe wasiwasi kuhusu Maliasili na Misitu tunachosema ni kwamba kuna wale ambao wanaopambana na Majangili wataendelea kuwa na Uni-form wataendelea kuwa na silaha kwa kadri ya uzito wa majukumu lakini kwa hawa wengi ambao wapo maofisini kama mfano mtendaji kwanini avae kama Mwanajeshi”
“Kuhusu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kukamata ni kweli Wananchi wamelalamika sana na niwaambie ukweli tu kuna mahali Mtu kasema kwamba ‘DC anammezea mate Girlfriend wako, anakusweka ndani Ijumaa hutoki mpaka Jumatatu’, sasa tunachosema yake Mamlaka waliyopewa Ma-RC na Ma-DC yalikuwa na sababu tatizo sio wao kuwa na Mamlaka tatizo yanatumika vibaya mno”
“Halafu na hivyo sasa kila saa wanatembea na Vyombo vya Dola, Kamati za Ulinzi na Usalama kwanza tunachosema wale Sheria inawatambua kwamba ni Wenyeviti wa Usalama ile component ya Ulinzi haipo lakini unaona wanaitumia halafu kila wanakoenda hata shughuli ambayo haiitaji hizi Kamati lakini wako nayo lakini hawa Watu wa hizi Kamati wana majukumu yao ya msingi sasa kama kila siku anafuatana na DC majukumu yao ya msingi watafanya saa ngapi?”
“Kama ni Polisi pengine ile gari inahitajika kwenda kupambana na Wahalifu lakini Mkubwa anasindikizana na DC wanakwenda kukagua darasa , aah pale ile Kamati haiitajiki”
“Serikali itatathmini majukumu haya kama yanaweza kuondolewa ni vizuri lakini yakibaki wazingatie masharti kwasababu Sheria inayowapa madaraka haya imeeleza ni mazingira gani DC au RC unaweza kutoa amri ya kukamata Mtu na ukishamkamata lazima utoe taarifa kwa Hakimu lakini nyie mmesikia wanafanya hivyo!?”