Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji EWURA James Angelile amezungumza na Waandishi wa habari leo Julai 20, 2023.
“Hivi karibuni kumetokea changamoto hasa hasa pembezoni Mwa Nchi na Miji kuhusu upatikanaji wa mafuta ya Petrol tumeona ni vyema tukutane na tuwaeleze Wananchi kwamba kwa jumla Nchi ina mafuta ya kutosheleza mahitaji yetu”
“Takwimu tulizonazo toka tarehe 14 tuna kiasi cha Lita Milioni 169 cha mafuta ya Petrol ambacho yanatosheleza kwa siku 25”
“Tuna mafuta ya Diesel ambayo ndio yanatumika kwa wingi zaidi ya Lita 309 ambayo yanatosheleza mahitaji zaidi ya siku 30”
“Utajiuliza kwanini kumetokea changamoto pembezoni Mwa Miji na Nchi hilo ni swali nasi tunajiuliza tukawa tunajiuliza, sasa kuanzia jana tumepita kwenye Depot ya Lake Oil, Mount Meru, Tipa, Puma hawa ndio wasambazaji wakubwa mafuta katika Nchi yetu”
“Na tumejiridhisha kwamba kulikuwepo na changamoto kwenye Depot ya upangaji wa magari kwenye Depot, wapakiaji wakifika Depot wanaambiwa nendeni Depot nyingine huo muda wanashindwa kupeleka mahitaji ya mafuta kwenye eneo husika, tumekubaliana kwa Wauzaji wa mafuta, Wamiliki Depot, TBS wote wafanya kazi Saa 24 ili kuhakikisha spidi ya kupeleka mafuta kwenye changamoto inaondolewa, niwatoe hofu Wananchi mafuta yapo kulitokea changamoto”