Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya amedhani mechi ya hisani maarufu Daby ya Bunda kwa mahasimu wawili kati ya Bunda Kids na Amani zote timu ya Bunda mjini, ambapo timu ya Bunda Kids imeondoka na kiasi cha Tsh. 500,000 baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Amani ambao wao ameondoka na kiasi cha Tsh. 250,000, kutoka kwenye mfuko wa Ester Bulaya.
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Bunda na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wa Bunda mjini na maeneo jirani.