Mfalme wa Morocco Mohamed VI amesifu hatua ya Israel ya kutaka kufungua Ubalozi nchini Morocco akisema kuwa hii ni hatua muhimu iliyolenga kuboresha uhusiano wa muda mrefu.
Katika ujumbe ambao Mfalme aliutuma kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema kuwa Ufalme wa Morocco umepokea maamuzi haya ya kidiplomasia ya Israel kwa mikono miwili.
Mfalme Mohamed VI pia alidokeza kuhusu mahusiano mabovu ya kidiplomasia yaliyokuwepo baina ya mataifa haya mawili tangu December ya 2020 hali ambayo kwa sasa imekua tofauti baada ya uhusiano kuwa bora.
Uhusiano baina ya Israel na Morocco unatarajiwa kuendelea kuwa bora hali itakayohakikisha maendeleo yatokanayo na juhudi za serikali za nchi hizi huku ushirikiano wa kimataifa ukizidi kunawiri.