Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amefanya Ziara ya Kukagua Miradi ya Boost kwa ajili ya Ujenzi wa Shule za Msingi ambapo amesema hadi kufikia sasa wamefika wastani wa 95% ya ukamilishwaji wa Ujenzi wa Madarasa.
Aidha Kaji Amemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kutoa Fedha Jumla ya Shilingi 940,900,000 kwa Ujenzi huo wa Madarasa 30 na Matundu ya vyoo 42 katika wilaya ya Tanga, ambapo Kukamilika kwa miradi hiyo itakwenda kuwasaidia Wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.
Pia Kaji amewapongeza Watendaji kwa Usimamizi mzuri wa Miradi hiyo hadi kufikia 95% ambapo ametoa wito kwa Watendaji wote kuhakikisha miradi yote katika wilaya hiyo inasimamiwa kwa ukaribu ikiwa ni pamoja ja kuonekana kwa Thamani ya Fedha zilizotolewa katika mradi husika.