Mwenyekiti wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Mohamed Kawaida amemuomba msajili wa vyama vya siasa nchini kiwachukilia hatua vyama na watu ambao wamekuwa wakitoa maneno ya sio faa kwa mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa majadiliano wa sakata la mkataba wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jiji la Arusha wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo wakati wa kutoa elimu kwa wakazi wa kanda ya kaskazini kuhusu makubaliano ya ushirikiano wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.