Wasichana 150 wenye umri kuanzia miaka 14_25 ambao wamepata ujauzito na kujifungua watoto wakiwa nje ya ndoa kupatiwa mikopo na elimu ya Kilimo cha Maua Manispaa ya Morogoro.
Wasichana hao ambao waliowengi wamekua tegemezi kwa wazazi wao baada ya wanaume wao kuwatelekeza kunufaika na elimu hiyo baada ya wadau wa maendeleo kupitia Mradi wa Nexis Digital Flower kutekelezwa kwwenye kata tatu za Manispaa ya Morogoro ambazo ni Bigwa,Magadu na Mindu.
Meneja Mradi huo NEXIS DIGITALI FLOWER Neema Shukuru amesema asilimia kubwa ya mabinti waliozaa wakiwa bado kwa wazazi inaoneshwa wanapitia manyanyaso na taabu wakati wa kupambania fursa mbalimbali za kupata kipato na kujiinua kiuchumi na kusababisha wengi wao kutumia njia zisizo rasmi kuingizia kipato, mabinti hao wameshauriwa kujikita katika kilimo cha maua.
Dokta Rachel Zakayo ni , Afisa mazingira wa mradi wa Nexis Digital Flowers anasema lengo la Mradi huo kuwawezesha wasichana hao kujipatia kipato na kuacha kufanya vitendo ambapo sio vya kimaadili ambapo wengi wao hufanya kwa tamaa ya Fedha.
Naye Sitta Banzi Mratibu wa mradi wa Nexis digital Flowers anasema licha ya wasichana hao kupatiwa elimu na mitaji lakini wataoata fursa ya kupata elimu ya kilimo kupitia mtandaoni kwa kutuma ujumbe wa maandishi na kupata majibu ya kitaalam bila malipo.
Zainabu Shambani ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo anasema Mradi umekuja muda muafaka kwani utakua mkombozi kutokana na changamoto za maisha wanazopata.
Anasema baada ya kupata ujauzito akiwa shule ya msingi kwa sasa amekua na maisha magumu kwani anakosa fedha za malezi ya mtoto na kumlazimu kupita mitaani kuomba hivyo Mradi huo utamuwezesha kujikomboa katika wimbi la ombaomba mtaani.