Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani imetoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wanawake 71 wa nafasi za juu SIWOLEMA za uongozi kutoka taasisi za Umma, sekta binafsi na taasisi zisizo za kiserikali nchini ili waweze kujiamini katika nafasi mbalimbali za uongozi walizopewa.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo ya siku Tano ya kuwajengea uwezo viongozi hao Wanawake nchini katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere, Kibaha Mkoani Pwani na kuhudhuriwa na washiriki kutoka CRDB, NMB, NSSF, TTCL, PSSF, Mkombozi Bank, USAF, TAMESA.
Mkuu wa Shule hiyo Prof. Marceline Chijoliga amesema Mafunzo hayo ya kuwakutanisha kuwajengea uwezo viongozi wanawake wa ambao wanauzoefu wa uongozi sio chini ya miaka mitano yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ambapo pia wamefundishwa mbinu Bora za uongozi wa utawala Bora katika taasisi wanazoongoza.
Amesema mafunzo hayo kwa viongozi wanawake Mameneja yalianza tarehe 17 Julai, 2023 hadi tarehe 22 Julai 2023, ikiwa ni muendelezo wa mafunzo mbalimbali yanayotolewa na Shule ya Uongozi kwa kushirikiana na taasisi za Umma, sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali na Chama Cha Mapinduzi.
Amesema tatizo linalowakabili Wanawake wengi viongozi hawajiamini katika nafasi zao za uongozi walizoaminiwa serikalini na kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambao hudiliki hata kukubali kuwapisha wanaume madarakani.
“Wanawake wengi ni wasomi wazuri na wanauwezo wa kufanya kazi nzuri katika nafasi walizoaminiwa lakini kwa kutojiamini kuongoza hukubali waongozwe na wanaume”
“Wapo Wanawake wanaambiwa tunakupa nafasi hii wanaogopa kuchukua ile nafasi ukimuuliza sababu anasema Mimi siwezi, unamuuliza mbona umesoma sawa kushika nafasi hiyo hakubali”
“Sisi Wanawake ni waajabu sana tunaweza kupata hizo nafasi lakini tukawa tayari kufanya kazi kwa kusaidia kiongozi mwanaume ambaye ana kiwango cha elimu na yeye lakini kuchukua nafasi hiyo ya uongozi hayupo tayari kufanya kwani kundi hilo limekuwa nyuma sana katika mambo mengi hata kufanya maamuzi”
Amesema pia kuna baadhi ya Wanawake hata kujiendeleza kielimu hawataki kwa kigezo cha majukumu ya familia hivyo hata Kuna baadhi ya vyeo hawezi kufikia hivyo Mafunzo hayo watawajengea uwezo viongozi hao Wanawake kwamba nini wafanye kwenye majukumu yao ya familia na majukumu ya kazini.
Alisema Mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia nini wafanye katika uongozi maana tunaaamini mwanamke kiongozi akiendelezwa atasaidia familia yake kwa kuwa kiongozi bora bali pia anakuwa kiongozi bora katika mazingira yake ya kazi”
Aliyataja masomo waliyofundishwa kuwa ni pamoja na uzalendo ambao huwapa kujitambua kuwa wao ni waafrika hivyo tunawajibu wa kuhakikisha Afrika inabadilika, utawala Bora kwani Wanawake tunaaminika ni waaminifu hivyo tunaendelea kupanda mbegu ya uaminifu kwa Wanawake wengi zaidi.
“Ikiwa ni pamoja na kuendesha miradi ya maendeleo, kujiamini, kushirikiana na wenzao kazini ikiwa ni pamoja na kufanya majadiliano ya wanawake kwa
Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania, Christine Musisi, akifunga mafunzo hayo ya uongozi kwa viongozi wanawake amesema Shiriki la Umoja wa Mataifa la programu ya maendeleo Tanzania linapongeza juhudi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi imara wa Raisi wa kwanza mwanamke Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa Uongozi wa wanawake na ushiriki wao katika ngazi za maamuzi katika ngazi zote za maamuzi serikalini.
“Tunatambua ongezeko la idadi ya viongozi wanawake bungeni, taasisi za umma na katika ngazi mbali mbali za utawala serikalini”
“Tunapongeza wanawake majasiri ambao wana-onyesha umahiri mkubwa na ujasiri katika kufanya maamuzi yanayo-husu Taifa, familia na jamii inayo-wazunguka pamoja na changamoto nyingi za kijinsia, kifamilia, kiuchimi na kihisia zinazo-wazunguka tofauti na wanaume”
“Hakika mwanamke akiwa katika kiti cha maamuzi basi ni rahisi kuundwa sera, mikakati na mipango inayo-wanu-faisha wanawake wengi zaidi; na mwanamke akifanikiwa kiafya, kielimu na kiuchumi basi jamii na Taifa kwa ujumla litakuwa limefanikiwa”
Amesema UNDP Tanzania itaendelea kushirikiana na taasisi za serikali zinazotoa mafunzo ya Uongozi kwa wanawake kama Mwalimu J.K Nyerere Leadership School, Uongozi Institute pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kama vile Tanzania Gender Network Program na sekta binafsi ili kuchangia ongezeko la idadi ya wanawake wenye uwezo na ujasiri wa kuongonza na kushawishi mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisera na kijamii hapa nchini.
Barozi wa Africa kusini nchini Noluthande Mayende Malepe amesema Kupinga ubaguzi wa rangi na mapambano ya kupata uhuru ilikuwa ni kipaumbele katika nchini yao lakini anafurahishwa na hatua kubwa ya Tanzania hata kutoa nafasi ya juu kabisa kwa mwanamke kwa Dr. Samia Suluhu Hassan.