Young Africans SC kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewaalika Klabu ya Kaizer Chiefs kutembelea Visiwa vya Zanzibar kama sehemu ya utalii katika visiwa vyenye vivutio bora.
Msafara huo ambao unangozwa na Rais wa Young Africans Eng.Hersi Said kwa uenyeji wa Makamu wa Rais Arafat Haji wakiwa na Wageni wao chini ya BOBBY KAIZER utatembelea maeneo kadhaa ya vivutio na historia ya visiwani Zanzibar
Na Julai 23, 2024 Kikosi hicho cha Kaizer Chiefs kilifanikiwa kufika nyumbani kwa Mama Fatma Karume ambaye ni mjumbe wa kudumu wa baraza la wadhamini Young Africans SC.
Wageni hao walipata wasaa na Mama Karuma na kuelezewa moja kati ya sehemu kubwa ya historia ya Young Africans na nchi yetu.