Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi pingmizi, ambapo katika hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350 wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama na watoto.
Uongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Suma Fyandomo, amesema katika mapambano hayo ya vifo vitokanavyo na uzazi wanamtambua Rais Samia kama askari namba moja mkoani humo kutokana na uimarishaji wa huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa vifaa.
Akizungumza jana katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe mkoani humo Suma amesema wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa kuendelea kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi ambapo katika hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350 wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama wao na watoto.
Alisema katika mapambano hayo wanamtambua Rais Dk.Samia kama shujaa na askari namba moja aliyedhamilia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini.
“Mkoa huu ni kati ya mikoa ambayo watu wanazaliana kwa wingi na hapo awali huduma za afya hususani za uzazi zilikuwa ni changamoto katika vituo na hospitali zetu lakini kwa sasa hususani miaka miwili hii ya Rais Dk.Samia tumeona uthubutu na uchungu alionao kwa wanawake wenzie ambapo vifaa tiba na mazingira wezeshe ya klujifungulia yanatuma uhakika wa kuwapo kwa uzazi salama,”alisema.