Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini James Kaji amesema Wasafirishaji wa Huduma za Bodaboda pamoja na Bajaji wataanza kutumia Vituo vinavyotambulika kwa namba sambamba na kuvaa Kiakisi (Reflector) zenye namba watakazokuwa wanatumia pindi wanapokuwa Barabarani ili kupunguza uhalifu ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya Vijana ambao wamekuwa wakifanya uhalifu kwa kutumia Bodaboda na kushindwa kutambulika.
DC James amesema hayo wakati akihitimisha kikao na Madiwani wa Jiji la Tanga ambapo amesema wamekubaliana na Uongozi wa Bodaboda na Bajaji Jijini Tanga kutambulika kwa namba pamoja na vituo vyao ili inapotokea uhalifu au abiria kusahau mzigo, Bajaji hiyo iweze kutambulika kwa haraka pamoja na kulinda usalama tofauti na sasa ambapo Bajaji hazina utambulisho wowote.
Amesema utekelezaji huo utaanza mara moja ambapo atakutana tena na Uongozi wa Bodaboda ambao tayari wamekamilisha mchakato wa katiba kwa ajili ya kuanza kwa utekelezaji huo.
VITUO VYA BODA NA BAJAJI KUPEWA NAMBA ILI KUZUIA UHALIFU TANGA