Bronny, mmoja wa wana wa gwiji wa NBA LeBron James, mtoto mkubwa wa mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, yuko katika hali nzuri baada ya kupata mshituko wa moyo, msemaji wa familia hiyo amesema.
Taarifa zinasema alipatwa na mshtuko wa moyo wakati wa mafunzo katika Chuo Kikuu cha Kusini mwa California (USC) Jumatatu.
‘Jana, wakati akifanya mazoezi, Bronny James alipatwa na mshtuko wa moyo. Wafanyakazi wa matibabu waliweza kumtibu Bronny na kumpeleka hospitali’
“Sasa yuko katika hali shwari na hayuko tena ICU,” mwakilishi wa familia alisema Jumanne.
“Wahudumu wa afya waliweza kumtibu Bronny na kumpeleka hospitali,” ilisema taarifa hiyo.
“Kwa sasa yuko katika hali nzuri na hayuko tena ICU (kitengo cha wagonjwa mahututi).”
Iliongeza: “Tunaomba heshima na faragha kwa familia ya James na tutavifahamisha vyombo vya habari wakati kuna habari zaidi.
Bronny ameorodheshwa kuwa mchezaji wa tano bora katika nafasi yake.