Mradi Mkubwa wa Maji wa Chamkorongo wenye Makadilio ya Thamani ya Shilingi Bilioni 6 Unatarajiwa kukamilika Mwezi September Mwaka huu ambapo Mradi huo unatarajiwa kuwafikia wananchi wapatao Elfu 68 Kwa wakazi wote wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro pamoja na Buselesele.
Akitolea ufafanuzi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita,(GEUWASA) Mhandisi. Frank Changawa amesema mpaka sasa Mradi huo umekamilika kwa asilimi 90 ambapo mpaka sasa mradi huo uko katika Majaribio ambapo amesema mradi huo upo katika hatua za awali za Majaribio.
“Tumekuwa tukitekeleza Mradi huu na Makadilio ya Ghalama ya Bilioni 6 lakini hadi sasa tumetumia Bilioni 4.7 na Mradi uko asilimia 92 kwa maana tumebakisha eneo la basic manaake Bomba kuu linalotoa maji katika tenki kama kilometa 2 kwa ajili ya kukamilisha maji yaanze kurudi kwenye tenki , ” Mhandisi Changawa.
Mhandisi Changawa amesema Mradi huo wanatarajia kutoa lita Milioni 2.5 kwa siku huku akibainisha Mradi huo kuwa nje ya mda ambapo amesema hali hiyo imepelekea kutokuwepo kwa Mabomba eneo husika huku akibainisha kusambaza maji katika maeneo kilometa 55 na kujenga Matenki mawili na moja likiwa la lita laki 5 na tenki la lita laki 150 pamoja na Busta Pointi.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji , Mhandisi .Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa na tayari wamekwisha laza kilometa zaidi ya 23 huku Kilometa 2 zikisalia katika kukamilisha Mradi huo ambapo ametoa maagizo ifikapo Mwezi Septemba mwaka huu Mradi huo uwe tayari umekamilika na kutoa huduma kwa wananchi.
Mhandisi Luhemeja amewataka wananchi kuwa subra wakati suala hilo likifanyiwa kazi ambapo pia ametembelea mradi wa Tenki la maji lililopo wilayani chato Mkoani Geita na kuangalia hali ya uzarishaji maji katika kituo hicho huku akikipongeza kwa kazi nzuri ambayo imewasilishwa na Meneja RUWASA wilaya ya Chato.
Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi , Luhemeja ni ya siku tatu katika Mkoa wa Geita ambapo atatembelea wilaya ya Bukombe na kukagua Miradi mbalimbali ya Maji pamoja na kuchanganua changamoto kutoka kwa Mamlaka husika za Maji.