Bunge la Ghana limepiga kura ya kufuta adhabu ya kifo, na hivyo watu 176, ikiwa ni pamoja na wanaume 170 na wanawake sita waliokuwa wanaosubiri kunyongwa wakiepuka adhabu hiyo, na kwa sasa watabadilishiwa adhabu na kukabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Ghana sasa imeongezwa kwenye orodha ndefu ya nchi za Kiafrika ambazo zimeondoa hukumu ya kifo katika miaka ya hivi karibuni.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa raia wengi wa Ghana wanaunga mkono kukomeshwa kwa hukumu ya kifo.
Mwaka jana, watu saba walihukumiwa kifo nchini Ghana – lakini hakuna hata mmoja wao aliyenyongwa. Uhaini pia ni uhalifu unaoadhibiwa kwa kifo nchini Ghana.
Ghana ilitekeleza hukumu ya kifo mara ya mwisho mwaka
Chanzo:RFI