Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka Wakazi wa Dar es Salaam kudumisha utaratibu wa kutunza mazingira na kuacha kutupa takataka hovyo huku akisema ameanza kutafuta Wadau ili wazichakate takataka na kutengeneza Mbolea, Nishati ya Umeme n.k ili kuepusha takataka kusambaa na kuchafua mazingira.
Amesema hayo wakati wa zoesi la kusafisha mazingira ya fukwe za Kigamboni (Pweza Beach) lililopewa jina la ‘Safisha Hifadhi Bahari’ ambalo limendaliwa na Chama cha MCs (TMCA)na TCC, zoezi hilo liliambatana na upandaji wa miti rafiki na mazingira ya Pwani na ugawaji wa vifaa vya uokoaji na utunzaji taka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo alitumia nafasi hiyo kuwataka Wana Kigamboni kutunza mazingira huku akisema Beach za Kigamboni ni miongoni mwa Beach bora nchini Tanzania hivyo zinapaswa kutunzwa kwa uchu mkubwa.
Zoezi hilo lilihudhuriwa pia na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Washereheshaji mbalimbali mashuhuri (MCs), Wafanyakazi na Viongozi wa TCC, Vyama rafiki na YMCA na Wadau wa Shisama, Mgeni rasmi, Wadau mbalimbali wa usafi na Wakazi wa Kigamboni.