Basi hilo lilikuwa likitoka katika mji wa kaskazini mwa nchi mnamo tarehe 26 Julai na liliripotiwa kuwa “limejaa kupita kiasi” likiwa na watu 76 yani watu 16 zaidi ya nambari inayoruhusiwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Senegal, Antoine Félix Abdoulaye Diome, alisema msongamano ni tatizo kubwa.
“Ningependa kutulia kwa muda ili kusikitishwa na ukweli kwamba bado kuna abiria wengi kwenye magari ya uchukuzi wa umma.
“Kwenye hati ya usajiri wa gari lililopata ajali imeelezwa kuwa idadi ya juu ya abiria ni 60.
“Hata hivyo, wahasiriwa walipohesabiwa, iligundulika kuwa kweli kulikuwa na watu 76.”
Abiria waliojeruhiwa walihamishwa hadi hospitali katika mji wa Louga na mji wa Saint-Louis.
Mnamo Januari, watu 19 waliuawa na 24 kujeruhiwa katika mgongano katika eneo hilo hilo, karibu na Louga.
Wiki iliyotangulia, karibu watu 40 walikufa wakati basi lilipoanguka katikati mwa Senegal.
Janga hilo, mnamo Januari 8, lilisababisha wimbi la ukosoaji dhidi ya mamlaka juu ya mara kwa mara ya ajali katika barabara za Senegal na ukosefu wa hatua zilizochukuliwa kuzizuia.
Serikali ilijibu kwa kutangaza orodha ndefu ya hatua, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku kwa safari za usiku za basi. Lakini wataalamu wa usafiri walisema hatua nyingi hazikuwa za kweli.
Hata hivyo, Diome anaamini hatua lazima ichukuliwe kuokoa maisha.
“Tangu baraza la mawaziri mnamo Januari 2023, kumekuwa na kupungua kwa ajali, kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya utawala,” alifafanua.
“Lakini pamoja na mkutano wa [Jumatano], tuna sababu ya kuamini kwamba kazi hakika inafanywa, lakini itabidi iendelee kwa uthabiti mkubwa zaidi katika hatua fulani.”