Polisi nchini Uganda wanachunguza Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Kawempe baada ya wanandoa kuhoji hali ya kifo cha mtoto wao mchanga ambaye uso wake daktari katika kituo hicho aliripotiwa kusema kuwa “uliliwa” na panya.
Wazazi hao, Yvonne Ainembabazi mwenye umri wa miaka 20 na mumewe Sulaiman Waiswa, 30, wanadai kuwa mtoto wao wa kwanza huenda alikuwa mwathirika wa dhabihu na jeraha kubwa upande wa kushoto wa uso lilikuwa haliendani na kuumwa na panya.
Bw Fred Mutebi, babu wa marehemu, alisema daktari ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kisheria, jioni hiyo aliwazuia wazazi hao bila maelezo kuuona mwili wa mtoto wao aliyekufa — katika chumba cha watoto na katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Wanandoa na jamaa walipofika asubuhi iliyofuata kuuchukua mwili huo, waliona jeraha kubwa la ajabu usoni na daktari yuleyule akawaambia, “mlifanya vibaya kumwacha [maiti] bila jeneza. Panya wamekula paji la uso la mtoto.”
Tazama zaidi…