Seke seke la usajili wa kiungo wa kimataifa wa Spain anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya La Liga limechukua hatua nyingine.
Fabregas ambaye anapiganiwa na vilabu vya Arsenal, Manchester United na Chelsea anatarajiwa kuuzwa baada ya kocha wake mpya Luis Enrique kuripotiwa kutokuwa na mpango nae kwenye utawala wake mpya Camp Nou.
Huku vita kubwa ikiwa inaendelea miongoni mwa vilabu vinavyomtaka, Katika mkutano wa waandishi wa habari wa timu ya taifa ya Spain inayojiandaa na michuano ya kombe la dunia, beki na mchezaji mwenzie Fabregas, Gerard Pique alisikika akimwambia kocha mkuu wa timu ya taifa ya Spain kwamba Cesc anaondoka Barcelona, na taarifa hizo ameambiwa na Fabregas mwenyewe.
Mazungumzo ya Pique na Del Bosque yalifanyika dakika chache kabla ya kuanza kwa mkutano, huku wakiwa hawajui kwamba vipokea sauti vimeawashwa wakawa wanazungumzia uhamisho wa Cesc.
Pique alisikika akisema: “Cesc Fabregas ameniambia uhamisho umekamilika, ameniambia amenunuliwa kwa Paundi milioni 33.”
Del Bosque akamjibu: “Maskini yule Rais (akimaanisha Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu). Hawezi kushinda namna.”
Katika mazungumzo hayo wawili hao hawakuitaja timu ambayo Fabregas ataenda kati ya timu zinazomtaka.
Angalia mazungumzo hayo hapa