Waziri wa ulinzi wa Urusi aliaongozana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kwenye maonyesho ya ulinzi ambayo yalikuwa na makombora ya balestiki yaliyopigwa marufuku ya Kaskazini huku majirani wakiahidi kuimarisha uhusiano, vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini viliripoti Alhamisi.
Waziri wa Urusi, Sergey Shoigu, na wajumbe wa China wakiongozwa na mwanachama wa Politburo wa Chama cha Kikomunisti waliwasili Korea Kaskazini wiki hii kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 70 ya kumalizika kwa Vita vya Korea, vinavyoadhimishwa nchini Korea Kaskazini kama “Siku ya Ushindi”.
Makombora hayo yenye uwezo wa nyuklia yalipigwa marufuku chini ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaliyopitishwa kwa msaada wa Urusi na China. Lakini wiki hii, walitoa hali ya kustaajabisha kwa kuonyesha mshikamano wa nchi tatu zilizounganishwa na ushindani wao na Marekani na kufufua kile ambacho baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa muungano wao wa zama za Vita Baridi.
Ziara ya Shoigu ilikuwa ya kwanza kufanywa na waziri wa ulinzi wa Urusi nchini Korea Kaskazini tangu kuvunjika kwa Muungano wa Sovieti mwaka 1991.Kwa Korea Kaskazini, kuwasili kwa wajumbe wa Urusi na China kunaashiria ufunguzi wake mkubwa wa kwanza kwa ulimwengu tangu janga la COVID-19.