Ahsante kwa kufuatilia matangazo yetu hii leo na jioni njema!
Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo kati ya pande hizo mbili, inaonekana makubaliano yamepatikana, na winga huyo wa Nigeria anajiunga na Milan katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani na kulingana na ripoti nyingi, Milan na Villarreal wamekubaliana juu ya mkataba wa €20m pamoja na €8 katika nyongeza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Milan msimu huu wa joto, baada ya kupata mikataba ya Marco Sportiello, Ruben Loftus-Cheek, Luka Romero, Christian Pulisic, Tijani Reijnders na Noah Okafor.
Mkurugenzi mpya wa michezo Geoffrey Moncada amekuwa na kazi nyingi ya kufanya msimu huu wa joto.
Uhamisho wa Sandro Tonali wa €70m ($77m) kwenda Newcastle umeipa Milan pesa nyingi zaidi za kufanya kazi nazo katika soko la uhamisho kuliko ilivyokuwa katika misimu kadhaa iliyopita, na hivyo Moncada amekuwa akifanya mazungumzo na vilabu vingi kwa ajili ya wachezaji.