Ni Julai 28, 2023 ambapo Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa anazungumza muda huu kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa Clouds FM 88.5.
“Majadiliano yote yanayotokea wakati huu yana umuhimu wake na hii ni kazi nzuri ya Rais Samia. Tumpongeze kwa hilo kwa sababu kipindi cha nyuma ulikuwa huwezi kusema kwa uwazi.” Jerry Silaa Mbunge Ukonga.
“Tumesema IGA hii ni mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Tanzania na Falme ya Dubai na ibara ya 2 (1) inaeleza kuwa nia hasa ni kutengeneza msingi wa kisheria wa ushirikiano’-
“Sasa huo ushirikiano unatajwa ibara ya 4 (1) kwa awamu ya kwanza na ya pili, na kinachotajwa ni ushirikiano sio miradi. Ukienda 5 (1) ndio inaeleza miradi itakayoanza ni ipi, ambayo ni Bandari ya Dar maeneo 7”
“Yapo makundi mawili, likiwamo lile linalopinga mkataba wa DP World kwa kusema ni wa ovyo, mfano neno territory kweli limo lakini halimaanishi alichosema Prof. Anna Tibaijuka (Hapa limemaanisha kuitambulisha nchi ya Tanzania). Sambamba na hayo kwenye mkataba huu wa makubaliano hamna sehemu ambayo inaeleza ‘kuuza’ bandari’,” Mbunge wa Ukonga.