Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilisema kuwa vikosi vya ulinzi vya Rwanda vilivuka mpaka wa Congo siku ya Alhamisi na kushambulia vikosi vya usalama vya mpakani na hivyo kuzidisha mivutano baina ya majirani wa kiafrika.

Mapigano yaliyofuata yaliwezesha Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) kuwazima magaidi wa Rwanda ambao walikuwa wamefanya uchochezi huo usiovumilika ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa waanzilishi wa shambulio hilo walirejea Rwanda.
Msemaji wa serikali ya Rwanda hakujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maoni yake.
Congo na Rwanda zimekuwa zikihusika katika mzozo tangu mwaka jana kuhusu kuzuka upya kwa kundi la waasi la M23, wanamgambo wanaofanya kazi mashariki mwa Kongo ambalo Kinshasa inaituhumu Rwanda kuwaunga mkono lakini Rwanda imekuwa ikikanusha hili mara kwa mara.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa pia wamesema wana ushahidi kuwa wanajeshi wa Rwanda wamepigana pamoja na M23 mashariki mwa Kongo na kuwapa waasi hao silaha na vifaa.