Fabinho anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Al-Ittihad siku chache zijazo huku Liverpool, wakisubiri kuangalia hati na hatua muhimu kisha makubaliano kufanywa kama ilivyoripotiwa hapo awali lakini Liverpool hivi sasa wanajiandaa kumenyana na Leicester City siku ya Jumapili katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya.
Hapo awali Fabinho alikuwa ameachwa nje ya kambi ya Liverpool ya kujiandaa na msimu mpya nchini Ujerumani huku mazungumzo yakiendelea kwa wiki chache sasa. Sasa atakaa nje safari ya Singapore ambapo Liverpool itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Leicester City na Bayern Munich.
Fabinho anatarajia kusaini mkataba wa £40m mkataba wa miaka mitatu ulikubaliwa na mchezaji huyo kwenda Al-Ittihad licha ya kuchelewa kwa makaratasi.