Ni Julai 30, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Mkoani Mwanza.
Hapa nimekusogezea Nukuu za Mkuu wa Wilaya ya Handeni Alberto Msando akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
“Mkataba wowote unaposainiwa, lazima uwe umesainiwa kwa jambo mahususi ambalo kila mtu anaweza kulifahamu. Kama ni kuuziana shamba, mkataba utasema tumeuziana Shamba, kama ni gari mkataba utasema tumeuziana gari’- Albert Msando, Mkuu wa Wilaya ya Handeni
‘Mkataba tuliosaini sisi unasema tutashirikiana kwenye mambo yaliyotajwa kwenye kiambatanishi namba moja. Hiyo unaipata kuanzia kifungu cha 1, cha 5, na kifungu cha 4. Kote huko ukipita utaona Kifungu cha 4 kinachopatikana ukurasa wa 15 kinasomeka hivi: Scope of Operation and Implementing entities’- Albert Msando, Mkuu wa Wilaya ya Handeni
‘Namba moja: The scope of this agreement is to facilitate the implementation of areas of cooperation set out in Appendix 1 to this agreement. Maaana yake kwa Kiswahili: mawanda/maeneo ya kushirikiana katika mkataba huu yametajwa katika kiambatanishi namba moja ambacho ni sehemu ya mkataba. Hauwezi ukausoma mkataba huu ukawa umekamilika bila kusoma kiambatanishi namba moja. Huwezi’- Albert Msando, Mkuu wa Wilaya ya Handeni
“Kimbatanisho hiki kinataja maeneo 7 mahususi ya bandari ya Dar ambayo kwa kifupi ni (1) Gati 0, 1-4, 5-7 za bandari; (2) kituo cha majahazi na abiria kitakachoendeshwa na TPA; (3) bohari ya kontena ya Kwala na lango la awali la bandari ya kurasini; (4) kituo kipya cha kontena na gati la mizigo ya jumla; (5) mifumo ya kisasa ya TEHAMA; (6) kutoa huduma za kisasa za hali ya juu (world class services); (7) mafunzo kwa wafanyakazi wa bandari”. Albert Msando, Mkuu wa Wilaya ya Handeni