Mkutano usio kuwa wa kawaida unafanyika Jumatatu, Julai 31 huko Jeddah kati ya nchi za Jumuiya ya ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu (OIC) juu ya suala la kudhalilisha Quran nchini Sweden na Denmark.
Katika miji ya Stockholm na Copenhagen, visa kama hivi vya kudhalilisha vitabu vya kidini vimepangwa kufanyika katika siku chache zijazo.
Denmark na Sweden zimetangaza kwamba zinatafuta suluhu za kisheria ili kukomesha visa hivi, ambavyo vimezua mvutano na nchi za utamaduni wa Kiislamu, pamoja na “hali ya hatari”, kulingana na Sweden.
Serikali ya Denmark inasema itachunguza njia zote za kisheria ambazo zinaweza kufanya iwezekane kupiga marufuku baadhi ya maandamano ambayo huenda yakazua mambo mengine nchini humo. Hii kwa njia maalum kabisa, na bila kuathiri uhuru wa kujieleza unaolindwa na Katiba.
Ili kuhalalisha masuala yasiyokubalika kwa sheria hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark amekumbusha kwamba udhalilishaji huu unafanywa na “watu wachache”, ambao lengo kuu ni “kuchochea chuki, kuleta mgawanyiko, kuwa na msimamo wa watu wenye itikadi kali”.
Wakati huo huo, kulingana na kura za hivi punde, Wasweden na Wadenmark wanapendelea kwa kiasi kikubwa kupiga marufuku uchomaji wa vitabu hivi. Wakati huu huko Copenhagen na Stockholm, visa kama hivi vya kuchoma Quran vimepangwa kufanyika kuanzia Jumatatu na katika wiki zijazo.