Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) imeanza kujitangaza kibiashara kwenye channeli mbalimbali za Television za Kimataifa ndani ya DStv ambapo tayari matangazo yake ya kwanza kwenye mpango huo wa kuliteka soko la Afrika Mashariki na Kusini yameanza kuonekana kupitia CNN.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka hiyo Dr. George Fasha amesema kabla ya hapo ilizoeleka kuona matangazo ya Nchi nyingine tunazoamini ziko mbele kimaendeleo zikinadi biashara zao kupitia Television kubwa za kimataifa na sasa Tanzania imetinga ili kuvutia zaidi biashara za kimataifa kwa ukanda huo na kulikamata soko.
“Taasisi yoyote inayodhamiria kufanya biashara kimataifa lazima ijizatiti kwa viwango vya kimataifa na ijitangaze kwenye anga za kimataifa, tumedhamiria kulikamata soko la Afrika Mashariki na Kusini pamoja na Wafanyabiashara kutoka dunia nzima wanaotaka kuingia kwenye soko hili, huu ni mwanzo tu kuna makubwa yanafuata” amesema Dr. George Fash
View this post on Instagram