Wafanya Biashara wa Maduka ya Darajani Souk Visiwani Zanzibar Leo hii Jumanne wamefanya Mgoma wa kutotaka Kufungua Maduka yao ,ambayo wamekodishwa na Makao makuu ya Ccm Zanzibar
Taarifa zinadai kua Manispa ya Mjini imekua ikipita madukani humo na kutoa katazo la kueka Biashara zao nje ya Maduka ,Jambo ambalo wafanya Biashara Hao wameonekana kupinga Katazo Hilo hadi kufikia siku ya leo kuamua kufanya Mgomo Huo ambao uliomfanya mkuu wa Wilaya Dc Rashid Msaraka Kufika Darajani Souk
Mkuu wa Wilaya amewataka wafanya biashara Hao kufungua maduka hayo huku akitoa Ruhusu ya kueka Biashara zao nje ya Maduka kama awali walivyo kua wakiweka Biashara Hizo Sambamba na Kuwataka wasifike neo la watembea kwa Miguu.