Waziri wa viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji amewaagiza maafisa biashara kwenye halmashauri zote nchi nzima kufanya ukaguzi kwenye maduka yanayouza bidhaa ya sukari ili kujiridhisha iwapo wanauza kwa bei elekezi ya shilingi elf 2800 kinyume chake wasisite kuwachukulia hatua.
Dkt Kijaji ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo ametumia nafasi hiyo kuwatoa hofu Watanzania kuwa hakuna uhaba wa sukari nchini kwakuwa bidhaa hiyo ipo ya kutosha na bei haijapamda kama inavyodaiwa katika baadhi ya maeneo..
Hata hivyo waziri Kijaji amesisitiza kuwa bei ya sukari nchini ni kati ya elfu 2800 na elfu 3200 na kuongeza kuwa iwapo mfanyabishara yeyote atagundulika kuuza kwa bei zaidi ya hapo serikali haitasita kumchukua hatua kwakuwa anawaumiza wananchi.