Taasisi ya Salt imeanza harambee ya kutafuta zaidi ya shilingi milioni 765 ambazo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha mafunzo kwa watoto wenye matatizo ya ufahamu ikiwemo matatizo ya usonji, downsyndrome na mtindio wa ubongo ambao wanatajwa kuwa zaidi ya milioni sita nchini .
Hayo yamesemwa mapema hii leo Jijini Dar es salaam katika mkutano wa Waandishi wa Habari pamoja na Taasisi ya Salt Iliyochini ya Mkurugenzi Mtendaji Bi, Rebecca Hudson Lebi akiwa na Watendaji Wake.
” Watoto hao kwa sasa wanalelewa na kupatiwa mafunzo kupitia taasisi ya Salt wanauhitaji wa kituo hicho kufuatia nusu yao waliopo katika kituo cha Salt wamefanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kubakwa na kulatiwa na ndugu wa karibu wa familia bado wanahitaji kituo hicho ambacho endapo kitakamilika kitakuwa kikiwafundisha namna ya kuzalisha bidhaa kupitia viwanda 10 vitakavyo jengwa katika kituo hicho “. Amesema Mkurugenzi wa Salt.
Hata hivyo naye mzazi wa mtoto mwenye tatizo la usonji Bibie Abdallah pamoja na wajumbe wengine wa Taasisi hiyo wamewataka viongozi na wananchi kujitokeza katika matembezi ya hisani ya kusaidia kuchangia fedha hizo ambapo tukio litakalofanyika September 24 mwaka huu kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa majengo ya awali ya kuwasaidia watoto hao ambao zaidi ya 460 wamekosa kujiunga na kituo cha mafunzo cha salt.