Kwa mara kwanza Hospitali ya Kanda ya Bugando Jijini Mwanza imefanikiwa kutoa Huduma ya Matibabu kwa watoto wanaozaliwa na utumbo nje tangu juhudi za kutatua tatizo hilo zilipoanza kufanyiwa utafiti mwaka 2001.
Mkurungezi Mkuu wa Hospitali ya Kanda ya Bugando Dkt. Fabian Masaga amesema ni 15% tu ya watoto wenye matatizo ya kuzaliwa na utumbo nje ndio wanatibiwa na kupona huku 75% ya watoto wanaozaliwa na tatizo la utumbo nje wanapoteza maisha,
kutokana na hali duni za wazazi.
Kwa upande wake Mkurungezi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Sister Massenga amewataka wajawazito wenye umri chini (25) wafanye vipimo vya mionzi pindi wanapopata ujauzito ili kufahamu hali ya mtoto akiwa tumboni kama anadalili zozote za kuzaliwa na tatizo la utumbo nje ili hatua za kitabibu zifanyike mapema.