Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso amesaini nyongeza ya miaka miwili ya mkataba wake ambao utamweka katika klabu hiyo ya Bundesliga hadi 2026, timu hiyo ilisema Ijumaa.
Mhispania huyo ambaye alichukua mikoba ya klabu hiyo iliyokuwa ikisumbua Oktoba mwaka jana, aliiongoza Leverkusen kumaliza katika nafasi ya sita na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Europa msimu uliopita.
“Ninashukuru kwa imani hii ambayo Bayer 04 inaweka kwangu,” alisema Alonso, mshindi wa zamani wa Kombe la Dunia na Uhispania ambaye yuko katika wadhifa wake wa kwanza wa ukocha mkuu.
“Ukweli kwamba tuna mawazo na mwelekeo sawa katika masuala ya michezo unaonyesha ukaribu na imani kati ya wakuu wa klabu na mimi mwenyewe.”
Leverkusen itacheza tena Europa League msimu huu.