Wizara ya mambo ya nje ya China imesema mazungumzo ya amani ya Ukraine nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma yalisaidia “kuunganisha makubaliano ya kimataifa”.
Mjumbe maalum wa China kwa masuala ya Eurasia, Li Hui, “alikuwa na mawasiliano ya kina na pande zote juu ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Ukraine alisikiliza maoni na mapendekezo ya pande zote, na kuunganisha zaidi makubaliano ya kimataifa”, wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa iliyoandikwa kwa shirika la habari la Reuters.
“Pande zote zilitoa maoni chanya juu ya kuhudhuria kwa Li Hui, na kuunga mkono kikamilifu jukumu chanya la China katika kuwezesha mazungumzo ya amani,” taarifa hiyo iliongeza.
Zaidi ya nchi 40 zikiwemo China, India, Marekani na nchi za Ulaya zilishiriki katika mazungumzo ya Jeddah yaliyomalizika Jumapili.
Urusi haikualikwa kujiunga na mjadala huo.