Tanzania imezidi kujidhatiti katika kuzalisha chakula kutoka tani 17,148,290 mwaka 2021/202/ hadi kufikia tani 20,402,014 mwaka 2023.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akihutubia mbele ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kilele cha Maonesho ya Kilimo Nane Nane, jijini Mbeya.
Waziri Bashe amesema kuwa zao la mahindi nalo limeongezeka katika soko la nje hadi kufikia tani 415,000 mwaka 2022/2023 kutok tani 223,000 mwaka 2021/2022. Ongezeko hilo ni kiashiria kuwa Tanzania inazidi kupiga hatua na nchi yenye kukidhi hitaji la chakula Barani Afrika.
Naye Rais Dkt. Samia amejidhihirishia hilo wakati alipotembelea mabanda ya watoa huduma mbalimbali kwenye Maonesho ya Nane Nane na kuhamasisha Taasisi husika kuzidi kutafuta soko ndani na nje ya nchi ili kupunguza wingi wa mazao yanayovunwa mavuno kutoka kwa wakulima.
Kwa mujibu ripoti za mwaka 2018 za Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo (FAO), ziada ya asilimia 60 ya chakula itahitajika kutokana na watu kuongezeka na kuwa nilionao 9.8 duniani hadi kufikia mwaka 2050.
Hivyo, Waziri Bashe ameeleza kuwa Serikali imezidi kuongeza mikakati mbalimbali ya uzalishaji kama vile Kilimo cha umwagiliaji, uchimbaji wa visima, upatikanaji wpembejeo na ubora wa mbegu ili uzalishaji wa chakula uzidi kuongezeka zaidi katika misimu ijayo.