Julen Lopetegui ameondoka rasmi Wolves kufuatia wiki kadhaa za sintofahamu kuhusu mustakabali wa meneja huyo huko Molineux na sasa Gary O’Neill, yuko kwenye mazungumzo ya kina ya kuwa meneja mpya wa Wolves baada ya uamuzi wa kuachana na Lopetegui Jumanne huku Wolves wakitarajia kusaini makubaliano hayo tayari leo.
Kuondoka kwake kunakamilika kwa miezi tisa katika klabu hiyo na kunakuja siku chache kabla ya Wolves kuanza msimu wao mpya wa Ligi ya Premia, huko Manchester United siku ya Jumatatu.
Meneja wa zamani wa Bournemouth Gary O’Neil anaweza kuchukua timu hiyo baada ya kuzungumziwa kuhusu nafasi hiyo endapo Lopetegui ataondoka.
Mustakabali wa Lopetegui katika klabu ya Molineux ulikuwa na uvumi tangu mwisho wa msimu uliopita alipoweka hadharani wasiwasi wake kuhusu mipango ya matumizi ya klabu.
Hali hiyo ilionekana kutatuliwa kufuatia mazungumzo na meneja huyo lakini Lopetegui aliweka wazi bado alikuwa na wasiwasi wakati wa mahojiano na Guillem Balague mwezi uliopita.
Alisema sio tu kwamba klabu ililazimika kuachana na Mpango A wa kuajiri lakini pia walikuwa wanatatizika kuandaa Mpango B. Klabu hiyo hadi sasa imekusanya takriban £90m kutokana na mauzo na imewasajili Matt Doherty na Tom King pekee, wote kwa uhamisho wa bure.