Bayern Munich wanatarajiwa kutuma ofa ya nne yenye thamani ya pauni milioni 94 kumnunua mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.
Hivi majuzi Spurs walikataa ofa ya pauni milioni 86 na Kane anataka mustakabali wake utatuliwe ifikapo Jumapili.
Dau lao linalofuata linatarajiwa kuwa la takriban £94m – £6m pungufu ya thamani ya Spurs iliyoripotiwa ya £100m.
Inaaminika kuwa Kane ana wasiwasi kuhusu kuondoka London Kaskazini msimu huu wa joto.
Na wakuu wa Spurs wanasemekana kuwa “wametulia” kuhusu hali hiyo.
Kane amekuwa nahodha wa Tottenham katika mechi zote tatu za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya chini ya Ange Postecoglou – akifunga mara nne katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Shakhtar Donetsk Jumapili.
Kwingineko Manchester City wanavutiwa na kiungo wa West Ham Lucas Paqueta na ripoti nchini Brazil zinadai kuwa mabingwa hao wa Premier League wametuma ofa ya pauni milioni 70.
The Hammers wanamfuatilia kiungo wa Southampton James Ward-Prowse lakini wanasitasita kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Brazil Paqueta.
Arsenal wanajipanga kumsajili mlinda mlango wa Brentford David Raya baada ya kuafikiana na mkataba wenye thamani ya £30m.